Monday 18 November 2019

MATUMIZI BORA YA MAJI KATIKA KILIMO CHA MPUNGA NO. 2

Utangulizi: Karibuni tena wanazinduka na kilimo na wapenzi wafuatiliaji wa makala bora za kuhusu maswala ya kilimo (ZINDUKA NA KILIMO BLOG) ambayo inatoa fursa ya kuelimika na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu maswala ya kilimo ikiwa ni hatua muhimu za kukabiliana na changamoto za kilimo tunazokumbana nazo siku kwa siku kama wakulima.

LEO: ni muendelezo wa somo la matumizi bora ya maji katika zao la mpunga.

Tumejifunza faida za matumizi ya maji katika zao la mpunga na zifuatazo ni muendelezo wa baadhi:-

  • Maji yakitumika kwa kidogo na kwa usahihi husaidia uongezwaji na ufunguliwaji wa vitivo na mashamba mapya ya mpunga na kuendelea kukuza vipato vya wananchi katika jamii husika.
  • Matumizi bora ya maji hupunguza gharama za uendeshaji na kuleta faida kubwa kwa mkulima hii ni kutokana na kupunguza idadi za uwekaji maji shambani pamoja na kupunguza bili za matumizi ya maji kwa baadhi ya skimu za mpunga hapa Tanzania (Water Right)

Hii picha ni mfano wa shamba linalofuata kanuni za matumizi bora ya maji
lipo katika skimu ya moshi 
MS 7-2 Block, Plot no 511










  • Sambamba na matumizi bora ya maji lakini pia kuna aina za mbegu za mpunga za muda mfupi na zinazo stahimili ukame na magonjwa pamoja na mavuno Mengi.
Baahdi ya aina hizo ni NERICA (NEW RICE FOR AFRICA) ambayo inaharufu nzuri, mazao mengi na inastahimili ukame, pia TXD 306 (Saro 5) ni aina ya mpunga inayofanya vizuri katika swala la mavuno mengi.

NB kipindi kijacho tutajifunza kwa undani kuhusu aina hizi mbili za mpunga na jinsi ya upatikanaji wakekwa watakao hitaji mbegu za mpunga.


Msisite kuuliza maswali kupitia blog na kupiga simu kwa ushauri na msaada kuhusu maswala ya kilimo na kuhitaji mbegu bora za mpunga
KIBAYA JASTINI SIMON, 
Mtariti wa mpunga, JIRCAS.
 +255 652397343


Wednesday 6 November 2019

MATUMIZI BORA YA MAJI KATIKA KILIMO CHA MPUNGA


Habari kwa wakulima wote wa zao la mpunga na wana zinduka na kilimo!!!

Leo tunawaletea somo muhimu la kutumia maji vizuri         
na kuendelea kupata mavuno mengi katika kilimo cha
mpunga.
Ni ukweli usiopingika kuwa wakulima wengi wa kilimo
 cha mpunga huamini kuwa shamba (boda) la mpunga
lililotuama maji wakati wote ndio lina sababisha kupata
mavuno mengi ya mpunga!
Laa hasha! ukweli ni kwamba kilimo cha mpunga kinahitaji maji ya wastani kabisa ili kusababisha mpunga katika ukuaji na mavuno yakutosha.

  •  Wakulima watambue kua kadiri urefu wa mpunga unapo ongezeka pia ndivyo na mizizi ya mpunga inazidi kukua kwenda chini hivyo maji yaliyotuama juu ya ardhi hayana matumizi katika mizizi iliyo ndani ya ardhi zaidi ya sentimita 25-40 kwakutegemeana na aina ya mpunga.
  • Pia maji yaliyotuama kwenye uso wa ardhi kwa muda mrefu pia huziba vijitundu vya hewa kwenye ardhi na kusababisha mmea kushindwa kupumua vivuri na kushindwa kukua na kuzaa vizuri.


Zipo sababu nyingine nyingi zilizofanyiwa utafiti na mashirika na taasasisi mbalimbali za tafiti za kilimo cha mpunga zinazoainisha hasara za maji yaliyotuama na faida ya maji yakunyweshea kwenya ardhi.

Leo tuishie hapo,
Tafdhali usikose muendelezo wa kujifunza na zinduka na kilimo juu ya matumizi bora ya maji katika zao la mpunga kwa wakati mwingine